TANGAZO LA MAHAFALI YA SABA YA KIDATO CHA NNE
Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi St. Gabriel unapenda kuwataarifu wazazi, walezi, wanafunzi, wahitimu, wadau wa elimu na jamii kwa ujumla kuwa shule inatarajia kufanya Mahafali ya Saba ya Kidato cha Nne.
Mahafali haya yatawakutanisha pamoja wanafunzi wahitimu, wazazi na walezi, walimu, viongozi, wageni waalikwa pamoja na wadau mbalimbali katika kusherehekea hatua muhimu ya safari ya elimu ya wahitimu wetu.
MAHAHALI HAYA YATAJUMUISHA:
Kuwapongeza na kuwaaga wahitimu wa Kidato cha Nne.
Tuzo na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo na maeneo mbalimbali.
Hotuba na nasaha kwa wahitimu kuhusu maisha yao ya baadaye.
Burudani na shughuli mbalimbali za mahafali.
Shukrani kwa wazazi, walezi, walimu na wadau kwa mchango wao katika elimu ya wanafunzi.
Tarehe: 10/10/2026
Muda: 08:30 Asubuhi - 03: 00 Mchana
Mahali: Shule ya Sekondari ya Ufundi St. Gabriel
Tunawakaribisha kwa moyo mkunjufu kushiriki nasi katika tukio hili muhimu na la kihistoria la Mahafali ya Saba ya Kidato cha Nne.
“ELIMU, UFUNDI NA MAADILI KWA MAENDELEO YA JAMII.”
Karibuni sana katika Mahafali ya Saba ya Kidato cha Nne – St. Gabriel!
Imetolewa na:
UONGOZI WA SHULE YA SEKONDARI YA UFUNDI ST. GABRIEL
Veyula – Dodoma