Ndugu wazazi/walezi wa wanafunzi wote TUMSIFU YESU KRISTO!
Uongozi wa shule unaendelea kumshukuru Mungu kwa kuendelea kutusimamia na kutulinda.Kidato cha kwanza na cha Tatu tupo salama tunaendelea vizuri .
Siku ya Alhamisi Tarehe 03/9/ 2026 wanafunzi watafunga Shule kwa likizo fupi na wataondoka siku ya Ijumaa Tarehe 04/9/2026 Hivyo wazazi waliopo nje ya DODOMA Jiji mtume nauli kuanzia kesho Tarehe 26/ 8/2026 namba ya kupokea nauli ni 0759156716.Jina EXUPERY LYIMO.
Wazazi mliopo DODOMA Jiji,mtawafuata wanafunzi Tarehe 04/9/2026 kuanzia saa 2:00Asubuhi hadi saa 4:00Asubuhi.Zigatieni muda. Hivyo uongozi wa Shule unaendelea kuwakumbusha Malipo yote ikiwemo Ada, kwa kwa wale ambao hawajakamilisha michango walipe kabla ya kufungua Shule. Kwa wanafunzi wa bweni wataanza kuripoti kuanzia Tarehe 13/09/2026 siku ya jumapili na wanafunzi wa kutwa wataripoti Tarehe 14/9/2026 siku ya jumatatu wakiwa na mahitaji yote muhimu.
BY HEADMISTRESS.